Museveni: Mimi si mtumishi bali mpiganiaji wa uhuru

Rais Museveni wa Uganda
Image caption Rais Museveni wa Uganda

Rais wa Uganda amewaambia raia wa nchi hiyo kuwa yeye si mtumishi bali mpiganiaji wa demokrasia.

Museveni mwenye umri wa miaka 72, alikuwa akiongea wakati wa sherehe za kuadhisiha miaka 31 tangu chama chake cha National Resistance Movement, kuchukua madaraka katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

"Mimi ni mpiganiaji uhuru ninayejipigania mwenyewe pamoja na imani zangu. Mimi si mwajiriwa. Ikiwa akuna mtu anafikiri kuwa alinipa kazi, anajidanganya. Mimi ni mpiganiaji wa uhuru ambaye mnafiki kuwa anaweza pia kuwasaidia." alisema Museveni.

Bwana Museveni alishinda muhula wa tano uliokumbwa na utata mwezi Februari mwaka uliopita.

Mada zinazohusiana