Trump kuteua jaji anayepinga uavyaji mimba

Maandamano dhidi ya uavyaji mimba nchini Marekani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maandamano dhidi ya uavyaji mimba nchini Marekani

Makamu wa rais wa Marekani , Mike Pence, ameuambia mkutano wa watu wanaopinga swala la utoaji mimba kuwa rais Trump mwenyewe atamteua jaji wa mahakama ya juu mwenye msimamo mkali dhidi ya tabia ya utoaji mimba.

Sera ya mwanamke kujiamulia kuhusu swala la utoaji mimba iliidhinishwa nchini tangu 1973.

Bw. Pence, akizungumza huko Washington amesema mkondo huo utabadilishwa na utawala mpya uliopo sasa.

Ni hivi majuzi tu ambapo utawala wa Trump ulitangaza kukata ufadhili kwa mashirika yote duniani yanaoshughulika na kutoa huduma za afya ya uzazi ambazo zinajumuisha pia huduma za utoaji mimba.