Mapigano yarejea upya Sudan Kusini

Vita vyarejea upya nchini Sudan Kusini kati ya vikosi vya serikali na waasi walio watiifu kwa Riek Machar
Image caption Vita vyarejea upya nchini Sudan Kusini kati ya vikosi vya serikali na waasi walio watiifu kwa Riek Machar

Mapigano yamerejea nchini Sudan Kusini kati ya serikali na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa rais nchini humo Riek Machar.

Ripoti kutoka kwa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile zinasema kumekuwa na mapigano makali ndani na nje ya mji wa Malakal ,ambapo wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanawahifadhi watu walioachwa bila makao.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa haijulikani kwa kuwa vita hivyo vinaendelea.

Umoja wa Mataifa umezitaka pande hasimu kusitisha uadui na kutekeleza makubaliano ya amani ya mwaka 2015.