Trump na Putin wawasiliana kwa simu IS ikiwa ajenda kuu

Trump akiongea Putin kwa njia ya simu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump akiongea Putin kwa njia ya simu

Rais wa Marekani Donald Trump amempigia simu mwenzake wa Urusi Rais Vladimir Putin kwa mara ya kwanza tangu achukue hatamu za uongozi wa Marekani.

Maafisa wa Marekani wameelezea mazungumzo baina ya wawili hao kuwa hatua muhimu sana katika kuboresha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili , uhusiano ambao ulikuwa umezorota sana.

Kwa mujibu wa utawala wa Urusi mazungumzo hayo ya saa nzima yalitoa kipa umbele ya vipi kukabiliana na kuzorota kwa usalama kutokana na mashambulizi ya kigaidi.

Hata hivyo swala la kuondolewa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi halijagusiwa.

Urusi iliwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani ikishirikiana na mataifa ya umoja wa ulaya pale ilipoivamia na kulimegua jimbo la Crimea kutoka Ukrain, huku wakiendelea kuwaaunga mkono waasi wa mashariki mwa Ukrain wanaopigana na serikali ya Ukrain.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uhusiano kati ya Trump na Putin ulizua utata wakati wa kampeni