Mashua yatoweka na watu 31 Malaysia

Malaysia
Image caption Malaysia

Maafisa wa huduma za uokozi huko Malaysia wako katika shughuli kubwa ya kuitafuta mashua iliyotoweka katika ufuo wa pwani ya Borneo ya ikiwa na watu 31, wakiwemo watalii 28 raia wa China

Vikosi vya wanamaji vinatafuta eneo la mraba wa zaidi ya kilomita laki 13 huku wakitumia meli na helikopta kadhaa.

Mashua hiyo ilikuwa inaelekea kisiwa kimoja cha kitalii ikiwa na abiria wengi raia wa uchina , bahati mbaya ikakumbwa na dhoruba na mawimbi makali baharini.