Watu 45 wafariki kwenye ajali Madagascar

Manusura wamepelekwa katika hospitali za karibu
Image caption Manusura wamepelekwa katika hospitali za karibu

Pametokea vifo vya watu wengi katika ajali nchini Madagascar baada ya lori lililokuwa limebeba watu waliotoka kwenye harusi kupata ajali na kuzama kwenye maji.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa takriban watu 45 wakiwemo watoto tisa na wanandoa wa harusi hiyo wamefariki.

Zaidi ya wengine 20 kwenye gari hilo wamenusurika.

Meya wa eneo hilo amesema kuwa chanzo halisi cha ajali hiyo bado hakijafahamika.