Sudan yapinga amri ya Trump

Rais wa Sudan Omar Bashir Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Sudan Omar Bashir

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Sudan imemuita mwanabalozi wa Marekani mjini Khartoum kupinga hatua ya Rais Donald Trump ya kuwapiga marufuku raia wa nchi hiyo kuingia Marekani.

Sudan inasema kuwa hatua hiyo ni ishara mbaya baada ya hatua nzuri za kuboresha uhusiano wa mataifa hayo mawili ikiwemo kupunguza vikwazo vya kiuchumi na ushirikiano katika vita dhidi ya Ugaidi.

Amri hiyo ya Trump ilitikiza mpango mzima ya wakimbizi wa Marekani baada ya kutangazwa marufuku ya siku 90 ya usafiri wa raia kutoka Somalia, Sudan, Libya, Syria, Iran, Iraq na Yemen.