Guterres aisifu Afrika kwa kuwakaribisha wakimbizi

Antonio Guterres Haki miliki ya picha AFP
Image caption Antonio Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesifu nchi za Afrika kwa kuwa kati ya nchi zinazowaruhusu wakimbizi wengi zaidi duniani kuingia nchi zao.

Bwana Guterres ambaye alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa muungano wa nchi za Afrika AU nchini Ethiopia, alisema kwa bara la Afrika limeiacha mipaka yake wazi wakati ambapo baadhi ya nchi zilizostawi zinafunga mipaka yao.

Matamshi yake yanatajwa na baadhi ya waandishi wa habari kuwa ya kushutumu amri iliyotolewa na Raia wa Marekani Donald Trump akipiga marufu wahamiaji kutoka nchi saba zenye waislamu wengi.