Sean Spicer awajibu wanadiplomasia

Marekani
Image caption Waandamanaji nchini Marekani wanaopinga sera mpya ya raisi Donald Trump

Kwa upand wake msemaji wa raisi wa Marekani, Donald Trump amesema kwamba wanadiplomasia waliomo nchini humo ambao wamekuwa wakilalamikia amri mpya inayozihusu nchi saba zenye itikadi ya dini ya kiislamu wanapaswa kuchagua kukubaliana na mpango huo ama kuondoka.

Sean Spicer alikuwa akijibu waraka uliotumwa kwenye ofisi yake na wanadiplomasia hao ambao unaeleza wazi kuwa sera hiyo mpya inayotaka kuifunga mipaka ya Marekani itawaathiri mamilioni ya wasafiri halali kwa dhana ya kutaka kuzuia magaidi wachache.

wanadiplomasia hao wameendelea kueleza kwenye waraka wao kuwa, hata wasafiri wasipoingia nchini Marekani, bado haitasaidia kuifanya nchi hiyo kuwa sehemu salama.

Hata hivyo mpaka sasa waraka huo haujaonekana hadharani lakini waraka huo BBC imebahatika kuushuhudia.

Wakati akizungumza katika Ikulu ya Marekani, Spicer amelalama kwamba wakosoaji wanapinga sera hiyo nje ya uwiano.