Morocco yarudi katika Umoja wa Afrika AU

Ramani ya Morocco
Image caption Ramani ya Morocco

Viongozi wa umoja wa Afrika wameamua kuirudisha Morocco katika shirika la Umoja wa Afrika AU zaidi ya miongo mitatu baada ya taifa hilo la ufalme wa Afrika Kaskazini kujiondoa katika AU kufuatia mgogoro wa eneo la Sahara magharibi.

Shirika hilo linatambui Sahara ya Magharibi kuwa jimbo huru, lakini Morrocco inasema kuwa eneo hilo ni mkoa wake wa kusini.

Morocco imepigania mpango wake wa kutaka kujiunga tena na Umoja wa Afrika mwaka uliopita.

Eneo la Sahara ya Magharibi linaendelea kuwa eneo tata ,lakini viongozi wengi wa Afrika walipiga kura kuikubali Morrocco kurudi katika Umoja wa Afrika.