Adebayor ajiunga na klabu ya Uturuki

Emmanuel Adebayor Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Emmanuel Adebayor

Mshambuliaji wa Togo Emmanuel Adebayor amejiunga na klabu ya Uturuki Istanbul Basaksehir kwa kandarasi ya miezi 18 kwa kitita kisichojulikana.

Mchazaji huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal, Manchester City na Tottenham mwenye umri wa miaka 32 alikuwa huru tangu aondoke Crystal Palace msimu uliopita.

Aliiwakilisha Togo katika kombe la mataifa ya Afrika mapema mwezi huu, lakini wakashindwa kufika katika awamu ya muondoano hivyobasi kumaliza wa mwisho katika kundi C.

Istanbul Basaksehir ni wa pili katika ligi ya Super.

''Alikuwa miongoni mwa wachezaji katika orodha yetu ya uhamisho ,alisema Mustafa Erogut.

Alirudi na ripoti nzuri na baadaye tukawasiliana na Adebayor.Mchezaji huyo anafurahia na mradi wa timu hii na maono ya rais wake kwa hivyo ni wazi kwamba klabu hiii na mchezaji huyu watasaidiana''.