Dawa ya Malaria yashindwa kuponya wagonjwa Uingereza

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Watu wanaotibiwa Uingereza ni wale husafiri nchi za kigeni

Dawa muhimu ya ugonjwa wa Malaria imeshindwa kuwaponya kwa mara ya kwanza wagonjwa wanaopata matibabu nchini Uingereza.

Dawa hiyo mchanganyiko haikufanikiwa kuwaponya wagonjwa wanne ambao wote walizuru bara la Afrika.

Kati ya watu 1,500 na 2,000 hutibiwa ugonjwa wa Malaria nchini Uingereza kila mwaka, hasa ya baada ya kusafi nchi za kigeni.

Wengi wao hutibiwa kwa kutumia dawa ya artemether-lumefantrine.

Lakini ripoti za hospitali zinaonyesha kuwa dawa hiyo ilishindwa kuwaponya wagonjwa wanne kati Oktoba mwaka 2015 na Februari mwaka 2016.

Wagonjwa hao walionekana kupata nafuu na kuruhusiw kuenda nyumbani, lakini wakalazwa baadaye wakati walionyesha dalili za ugonjwa huo tena.