Msichana wa miaka 10 ajilipua Nigeria

Kundi la Boko Haram limekuwa likitumia wanawake wenye umri mdogo kama washambuliaji wa kujitoa mhanga Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la Boko Haram limekuwa likitumia wanawake wenye umri mdogo kama washambuliaji wa kujitoa mhanga

Msichana ambaye anakisiwa kuwa wa umri wa miaka 10, amejilipua kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Walioshuhuida walisema kuwa msichana huyo alienda kwa kambi ya wakimbizi wa ndani kwenye mji wa Banki jimbo la Borno ambapo alisimamishwa na wanajeshi.

Wanajeshi hao walimtaka ainue hijabu yake ambapo waliona vilipuzi vikiwa vimefungwa kiunoni mwake. Msichana huyo kisha akajilipua.

Katika kisa kingine mtu mmoja aliuawa kwenye shambuliz la kujitoa mhanga kwenye mji wa Maiduguri.

Kundi la Boko Haram limekuwa likitumia wanawake wenye umri mdogo kama washambuliaji wa kujitoa mhanga kwenye maeneo yenye watu wengi kama kwenye misikiti, masoko na vituo vya mabasi.