Mapigano mapya mashariki mwa Ukrain

Mapigano mapya yanajiri wakatika wa kipindi cha baridi kali Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano mapya yanajiri wakatika wa kipindi cha baridi kali

Utawala nchini Ukraine umesema kuwa unachunguza uwezekano wa kuwahamisha maelfu ya raia kutoka maeneo ya mashariki mwa mji wa Avdiivka.

Utawala unasema unachukua hatua hiyo eneo hilo lililo takriban kilomita tano kaskazini mwa Donetsk, kufuatia kuongezeka kwa mapigano hali ambayo imesababisha upungufu mkubwa wa maji wa umeme.

Makombora ya roketi na silaha nzito nzito zimesikika na kuonekana tangu mapema hii leo.

Mji wa Avdiivka ambao unafahamika kutokana na viwanda vyake vingi, umekuwa kitovu cha mapigano tangu siku ya Jumapili.

Umeme umekatizwa mjini humo na kwa sasa hali ni baridi sana. Afisa anayesimamia baraza la mji huo, amesema kuwa anajianda kwa shughuli ya kuwahamisha raia kutoka mji huo.

Mjini moscow, msemaji wa raisVladimir Puttin, amesema kuwa wana habari za kuaminika kuwa makundi ya wapiganaji wanaounga mkono Ukraine ndio waliosababisha upya mapiganao hayo na wala sio jeshi.

Rais wa ukraine, Petro Poroshenko, ameelezea wasi wasi wake kuhusiana na ushindi wa Bwana Donald Trump, kuwa rais wa Marekani na hatua yake ya kumsifu kiongozi wa Urusi Vladimir Putin umechochea mzozo huo wa Mashariki mwa Ukraine.