Watu wasafiri kilomita 6 kutafuta choo Afrika Kusini

Watu wasafiri kilomita 6 kutafuta choo Afrika Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wasafiri kilomita 6 kutafuta choo Afrika Kusini

Ukosefu wa maji nchini Afrika Kusini umesababisha baadhi ya wafanyakazi kufunga safari ndefu hadi mji ulio karibua kutafuta choo.

Kulingana na mtando wa News 24, wafanyakazi katika idara ya maendelea ya kijamii mji wa Mpumalanga mashariki mwa nchi huendesha magari umbalia wa kilomita 6 kutafuta choo kwa haja kubwa.

Mjini Cape Town maafisa wanasema kuwa wenyenji na biashara bado zinatumia lita milioni 7 zaidi kila siku na wameonya watu dhidi ya kutumia maji kwa njia mbaya.

Wafanyakazi wa nyumbani wameshauriwa kutumia ndoo moja ya maji kwa wakati moja na kwa siku za Jumanne Jumamosi.