Trump atetewa sera ya kuzuia wahamiaji waislam

Kiongozi wa mambo ya ulinzi wa Marekani John Kelly
Image caption Kiongozi wa mambo ya ulinzi wa Marekani John Kelly

Kiongozi mpya wa masuala ya ulinzi wa Marekani Jenerali John Kelly ametetea sera ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump ya kuzuia raia wa nchi saba za kiislam kuingia Marekani.

Kelly amesisitiza kuwa kwa sasa wanahitaji kujitenga na magaidi kutoka kila pembe ya dunia.

Amesema kuwa japokuwa anaonekana kupingwa na wengi, lakini uamuzi huo ni kwa manufaa ya wamarekani wenyewe.

Mamia ya raia wa nchi hizo saba walikwama katika viwanja mbalimbali vya ndege baada ya Trump kutoa amri hiyo.