Tanzania: EAC ilimuunga mkono Amina Mohammed wa Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yasema ilimuunga mkono Amina Mohammed wa Kenya

Tanzania imepuuzilia mbali madai kwamba baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki hayakumpigia kura mgombea Amina Mohammed wa Kenya katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika.

Amina ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Kenya, alishindwa na mwezake wa Chad Moussa Faki Mahamat, ambaye sasa ni mwenyekiti wa AU.

Akizungumza na BBC jijini Addis Ababa, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga, amesema madai katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya kuhusu uchaguzi huo ni ya kupotosha.

Mahiga alizungumza na mwandishi wetu Emmanuel Igunza ambaye alianza kwa kumuuliza kuhusu shutuma hizo wakati wa uchaguzi wa viongozi wa AU.