Jamii ya Makonde yapewa vitambulisho Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Jamii ya Wamakonde yapewa vitambulisho Kenya

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo hii amewakabidhi jamii ya Wamakonde vitambulisho vyao katika kaunti ya Kwale, na kutekeleza ahadi yake ya mwaka jana Wamakonde walipomtembelea katika Ikulu ya Nairobi. Rais wakati huo alisema ni haki yao watambuliwe kama wenyeji kwa sababu walizaliwa nchini Kenya baada ya wazazi wao kuhamia huko miaka ya hamsini na kuajiriwa katika mashamba ya makonge. John Nene alikuwa huko na kuzungumza na baadhi ya jamii ya Wamakonde kutaka kujua jinsi maisha yao yamebadilika tangu watambuliwe kama Wakenya.