Je, ni ugonjwa wa kumea miti umemuathiri msichana huyu?

Madaktari wana matumaini kuwa ugonjwa wa Sahana hauna makali sana Haki miliki ya picha AFP
Image caption Madaktari wana matumaini kuwa ugonjwa wa Sahana hauna makali sana

Wakati vitu visivyokuwa vya kawaida vilipomea kwenye uso wa Sahana Khatum, mwenye umri wa miaka 10 miezi minne iliyopita, babake hakushikwa na wasi wasi.

Lakini wakati vitu hivyo vilianza kusambaa, alishikwa na wasi wasi na kumlazimu kutoka kijijini mwake na kuelekea mji mkuu wa Bangladesh Dakar, kutafuta matibabu.

Madaktari sasa wanahofu kuwa Sahana huenda akawa mtoto wa kike wa kwanza kukumbwa na tatizo linalojulikana kama "tree man syndrome".

Ikiwa uchunguzi utabainisha hivyo, atakuwa mmoja wa watu wachache duniani walio katika hali hiyo.

Ni hali ya kijenetiki isiyokuwa ya kawaida ambapo mti humea hususan kwenye mikono na miguu.

Ni watu wachache ambao wote ni wanaume wanaoaminiwa kuwa na ugonjwa huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakati kama huu mwaka uliopita Abul Banjar alikuwa ameugua sana ugonjwa huo

Mikono yote ya Abul Bajandar ilimezwa na miti iliyomea yenye uzito hadi kufikia kilo tano

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye alikuwa raia wa kwanza wa Bangaladesh kupatikana na ugonjwa huo, kwa saa amefanyiwa upasuaji mara 16 na anaweza kuitumia mikono yake.

Madaktari wale wale waliomfanyia upasuaji Abul Bajandar, tena wanaendesha uchunguzi kubaini ikiwa Sahana anaugua ugonjwa sawa na huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Babake Sahana Mohammad Shahjahan ana matumaini kuwa madaktari watamtibu mtoto wao