Amnesty International na kofia nyeupe

white helmet
Image caption Kikosi cha uokozi cha kofia ngumu nyeupe wakiwa kazini

Wafanyakazi wa shirika la Amnesty International, limezindua kampeni ya kudai kuachiliwa kwa wafanyakazi wa kikosi cha uokozi mwenye asili ya Syria ijulikanayo kama kofia ngumu nyeupe .

Shirika hilo liliarifu kuwa vikosi vya serikali walimkamata Abdulhadi Kamel alipokuwa kwenye gari iliyowabeba raia nje ya mashariki Aleppo mwezi Desemba, na mpaka sasa hakuna taarifa zinazomhusu mpaka kilipoonekana kipande cha video kilichorekodiwa kwa lugha ya kirusi kilichowekwa katika mtandao wa Youtube kilichomwonesha akilaani kampeni ya kofia ngumu nyeupe na kudai kuwa ni kama propaganda za shirika hilo.

Familia ya Abdulhadi wanaamini kwamba mkuu wao wa kaya alilazimishwa kuyatamka maneno hayo na si kauli yake binafsi. Kufuatia video hiyo nalo shirika la Amnesty International limetoa wito kwa mamlaka ya Syria kutangaza hatma yake na kutaka kujua wapi alipo.