Iran yajaribu kombora la nyuklia

Marekani
Image caption Mshauri wa Marekani wa masuala ya Usalama wa Taifa la Marekani, Michael Flynn

Mshauri wa Marekani wa masuala ya Usalama wa Taifa la Marekani, Michael Flynn, amesema kwamba Marekani tayari inaifuiatilia kwa karibu Iran baada ya kufanya jaribio la komborala nukilia liitwalo ballistiska mwishoni mwa wiki.

Ingawa hajaweka bayana ni hatua gani zitafuata ama zitachukuliwa dhidi ya kitendo hicho.Na kulielezea jaribio hilo kama kitendo cha uchokozi, jenerali Flynn amesema Iran imekiuka maelekezo ya baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya silaha za nyukilia.

Ameongeza kusema kwam Iran inapata kiburi kwa kile alichokiita mikataba dhaifu kuhusiana na vinu vya nyukilia vya Iran na mpango wa nyuklia wa Teheran haukufikiwa na utawala uliopita wa rais Barack Obama na Umoja wa Mataifa.