Je, Etienne Tshisekedi ni nani?

Kiongozi wa upinzani nchini DR Congo Etienne Tshisekedi
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini DR Congo Etienne Tshisekedi

Akiwa mzaliwa katika jimbo la kati la Kasai mnamo mwezi Disemba mwaka 1932, bw Tshisekedi akiwa na umri wa miaka 79 alikuwa kiongozi wa upinzani mwenye umri mkubwa.

Alisomea sheria chini ya ukoloni nchini Ubelgiji.

Harakati zake za kisiasa zilianza wakati wa uhuru wa taifa hilo mwaka 1960 ambapo alikabidhiwa nyadhfa za juu katika serikali ya kati mbali na utawala wa Kasaian uliokuwa mfupi.

Mnamo terehe 14 mwezi Novemba 2011, akiwa waziri wakati wa serikali ya dikteta Mobutu Sese Seko bw Tshisekedi alijimwaga katika siasa za upinzani 1980 wakati Mobutu alipoamua kufutilia mbali uchaguzi wote.

Akiwa kiongozi wa chama cha muungano wa Demokrasia pamoja na chama cha Social Progrees, amekuwa mpinzani wa serikali zote tangu wakati huo.

Wakati Mobutu alipolazimishwa kutengeza serikali ya muungano na upinzani, bw Tshisekedi alikuwa waziri mkuu mara mbili katika kipindi cha miaka miwili.

Alijiuzulu nyakati zote hizo alipokosana na Mobutu.

Chama cha Bw Tshisekedi hakikushiriki katika vita wakati wa vita vilivyozuka baada ya utawala wa Mobutu kuanguka 1997, na hivyobasi kupata umaarufu mkubwa kutoka kwa raia walioathirika na mapigano hayo.

Baada ya kususia uchaguzi mwaka 2006, ambao anadai ulifanyiwa udanganyifu ,bw Tshisekedi aliamua kujitokeza na kuhakikisha kuwa anashinda.

Kwa wengine aliamua mapema kujitangaza kuwa rais kabla ya kupigwa kwa kura hiyo.

Raia wa Congo ni watu huru na wamenitangaza mimi kuwa rais, alisema wakati wa uzinduzi wa kampni yake mnamo tarehe 11 mwezi Novemba.

Wakosoaji wake wanasema kuwa ana taarifa zenye itikadi kali ambazo zinaweza kuchochea ghasia.

Tshisekedi ana umaarufu mkubwa katika jimbo la Kasai mjini Kinshasa.

Wafuasi wake na wale wa Kabila wamekuwa wakizozana katika misingi ya kikabila kusini mwa DR Congo ambapo raia wengi wa kasai wamehamia.

Chama chake cha UDPS kina umaarufu mkubwa kusini mwa taifa hilo lakini sio maeneo yote ya nchi.

Hivi majuzi kiongozi huyo alisafirishwa hadi nchini Ubelgiji kufanyiwa matibabu.DR Congo: Tshisekedi asafirishwa Ubelgiji kwa matibabu

Mada zinazohusiana