Mahakama kuamua kuhusu mpaka wa Kenya na Somalia

Mahakama kuamua iwapo ina uwezo wa kusikiliza kesi ya mpaka wa somalia na kenya baharini
Image caption Mahakama kuamua iwapo ina uwezo wa kusikiliza kesi ya mpaka wa somalia na kenya baharini

Mahakama ya kimataifa kuhusu haki, leo itatoa uamuzi wake wa iwapo ina uwezo wa kusikiliza kesi kuhusu mzozo wa mpaka wa baharini kati ya Kenya na Somalia.

Mataifa hayo mawili yanazozania eneo moja ndani ya bahari hindi linalodaiwa kuwa na utajiri mkubwa wa hifadhi ya mafuta na gesi .

Somalia inataka mpaka huo kupanuliwa kuelekea kusini, lakini Kenya inasema kuwa mataifa hayo mawili yalitia saini makubaliano ya swala hilo mwaka 2009 na hivyobasi hakuna umuhimu wa mahakama hiyo kuingilia kati.

Lakini bunge la Somalia limepuuzilia mbali makubaliano hayo