Maandamano dhidi ya serikali yafanyika Romania

Waandamana dhidi ya serikali Romania Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamana dhidi ya serikali Romania

Polisi nchini Romania, wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu wanaoandamana dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Bucharest.

Maandamano hayo yametajwa kuwa makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa utawala wa kikomunist mwaka 1989.

Ripoti zinasema hadi watu elfu mia mbili na hamsini, wameandamana kupinga amri ya dharura iliyotolewa na serikali kuhalalisha baadhi ya makosa ya ulaji rushwa.

Mataifa sita yakiwemo, Ujerumani, Ufaransa na Marekani yametoa taarifa ya pamoja kuionya Romania dhidi ya amri hiyo yakisema huenda ikahujumu sifa yake kimataifa na mahusiano ndani ya EU na NATO.