Mwanamuziki Beyonce atarajia kujifungua mapacha

Picha ya Instagram ya Beyonce Haki miliki ya picha Beyonce/Instagram
Image caption Picha ya Instagram ya Beyonce

Chini ya wiki mbili tangu Donald Trump aapiswhe kuwa rais wa Marekani, taarifa kuu kutoka Marekani tangu wakati huo zimehusiana na siasa.

Amri za Trump na mabadiliko kwa sera za Marekani vimeonekana kugubika masuala mengine yanayoibuka Marekani.

Kabla ya Trump kuapishwa, mashabiki wengine walidai kuwa Beyonce angetoa albamu mpya wakati Trump akiapishwa.

Hata hivyo Beyonce hakutoa albamu bali alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa angetoa vitu tofauti,

Haki miliki ya picha AP
Image caption Beyonce, mumewe Jay Z na binti wao Blue Ivy

Ukweli ni kwamba Beyonce ana ujauzito wa mapacha.

Picha ya Instagram ilimuonyesha Beyonce akiwa amepiga magoti kando na maua akionekana kuwa mjamzito.

Taarifa hizo za Beyonce zilionekana kuwavutia watu kutoka mitandao mingine.

Watu wengine wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu majina watakayopewa watoto wa Beyonce, wenginewakisema waitwe Yellow na Red Ivy. Binti wa umri wa miaka mitano wa Beyonce na Jay Z aliopewa jina la Blue Ivy Carter.

Haki miliki ya picha AFP

"