Makanisa kubomolewa Sudan

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Sudan Kusini Omar Bashir

Utawala nchini Sudan una mpango wa kubomoa makanisa 25 kwenye mji mkuu Khartoum, kwa mujibu wa mtandao wa redio moja iliyo nchini uholanzi ya Tamazuj.

Makanisa hayo yatabomolewa kwa madai kuwa yamejengwa maeneo ya makaazi.

Mtandao huo ulimnukuu kasisi Yahya Abdurrahman wa kanisa la Evangelican la Sudan, akiilamua serikali kwa kupanga kuharibu maeneo wanakofanyia ibada wakiristo.

"Hatua hii inalenga makanisa yaliyo mjini Khartoum kwa sababu kuna madai kuwa yako maeneo ya umma lakini nafikiri kuwa huo ndio mpango," alinukuliwa akisema.