Tsvangirai akosoa kukamatwa kwa mhubiri

Morgan Tsvangirai Haki miliki ya picha AFP
Image caption Morgan Tsvangirai

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amekosoa kukamatwa kwa mhubiri Evan Mawarire ambabe alizuiwa baada ya kurejea nchini humo siku ya Jumatano.

Bwana Mawarire alipata kwanza umaarufu mwezi Aprili wakati alichapisha video kwenye mtandao wa Facebook, akiwa amejifunga bendera ya Zimbabwe huku akilalamikia hali ya taifa hilo.

Video hiyo ilisababisha kutokea kwa kampeni ya kupinga uongozi wa nchi hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Evan Mawarire

Mhubiri huyo amefunguliwa mashtaka ya kuvuruga serikali iliyochaguliwa

Bwana Tsvangirai anasema kuwa mhubiri huyo hajatenda uhalifu wowote. Anasema kuwa watu wa zimbabwe hawawezi kuhangaishwa na chama cha Zanu PF.