Makamu wa Rais Kenya akana kumtelekeza mtoto

Haki miliki ya picha AFP
Image caption William Ruto

Nakala zinasombaa kwenye mitandao zinaonyesha kuwa Makamu wa Raia nchini Kenya William Ruto, anashtakiwa kwa kushindwa kuchangia malezi ya mtoto.

Nakala hizo zinasema kuwa Bwana Ruto ameshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake kama mzazi, wakati mlalamishi ambaye ni mamake mtoto akidaia ana haki ya kupata malezi kwa kuwa yeye hana uwezo wa kumlea.

Hata hivyo Ruto aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, akisema kwa mtoto wake wa umri wa miaka 11 anatunzwa vyema akiwataka watu wengine wakome kuingilia mambo hayo.