Walio na akili punguani kupokonywa bunduki Marekani

Wamiliki wa bunduki Marekani
Image caption Wamiliki wa bunduki Marekani

Bunge la uwakilishi nchini Marekani limepiga kura kuondoa sheria inayowaruhusu watu walio na akili punguani kumiliki bunduki.

Chini ya sheria hiyo iliopitishwa na utawala wa Barrack Obama uchunguzi wa kina utafanyiwa mtu anayetarajiwa kumiliki bunduki hiyo ambaye hupata ufadhili wa walemavu na ana matatizo ya kiakili.

Huwezi kusikiliza tena
Zuhura: Kufyatua risasi si mchezo

Mwenyekiti wa kamati ya haki Bob Goodlatte amesema kuwa sheria hiyo inabagua na kwamba hakuna ushahidi wowote kwamba watu walio na akili punguani wako hatarini mbele ya umma.

Rais Donald Trump alifanya kampeni na kuahidi kwamba Wamarekani wataendelea kumiliki bunduki.