Silaha za nyuklia: Marekani yaionya Korea Kaskazini

Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis na mwenzake wa Korea Kusini Han Min-koo Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis na mwenzake wa Korea Kusini Han Min-koo

Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa Korea Kaskazini itakabiliwa vikali iwapo itafanya utumizi wowote wa silaha za kinyuklia .

Bw Mattis yuko nchini Korea Kusini ambapo ameihakikisha Seoul Korea kwamba inaungwa mkono na Marekani.

Majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya nyuklia yanayofanywa na Korea Kaskazini mbali na taarifa za uchokozi yanaendelea kutia wasiwasi mbali na kuyakasirisha mataifa ya eneo hilo.

Marekani ina wanajeshi wengi nchini Korea Kusini na Japan ikiwa ni mpango wa ulinzi wa baada ya vita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Korea Kusini na wenzao wa Marekani wakishiriki katika mazoezi ya pamoja

Rais Donald Trump awali amenukuliwa akisema kuwa mataifa hayo mawili yanafaa kuilipa Marekani zaidi ili wanajeshi wake kusalia kukaa nchini humo.

Bw Mattis ametumia ziara yake nchini Korea Kusini kulihakikishia taifa hilo kwamba utawala wa bw Trump utaendelea kulinda eneo hilo.