Mwanajeshi wa Ufaransa ampiga risasi mshambuliaji mjini Paris

Oparesheni kubwa ya usalama inaendelea Haki miliki ya picha AP
Image caption Oparesheni kubwa ya usalama inaendelea

Mwanajeshi mmoja nchini Ufaransa ambaye alikuwa amelinda makavazi ya Louvre mjini Paris, amempiga risasi na kumjeruhi vibaya mwanamme ambaye alikuwa na kisu mkononi, aliyekuwa akitamka maneno"Allahu Akbar"

Mshambuliaji huyo anaripotiwa kujaribu kuingia eneo lenye maduka lililo chini ya ardhi nje ya makavazi hayo.

Ripoti zinasema kuwa alikuwa na mkoba lakini hakuna vilipuzi vilivyopatikana.

Oparesheni kubwa ya usalama inaendelea na wizara ya masuala ya ndani imetaja hali hio kuwa mbaya.

Polisi wanasema kuwa mwajeshi huyo alimfyatulia risasi tano mtu huyo ambaye alikuwa na kisu mkononi.