Beyonce kufanya tamasha akiwa mjamzito

Beyonce Haki miliki ya picha Beyonce.com
Image caption Beyonce

Beyonce atafanya tamasha wakati wa sherehe za tuzo za Grammy za mwaka huu, akiwa na ujauzito wa mapacha kwa mujibu wa babake Mathew.

Wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha runinga, alisema kuwa nyota huyo anaonekana akiwa na uchovu kwa sababu amekuwa akijiandaa kwa tamasha hizo.

Pia alisema kuwa alishtuka kusikia taarifa kuhusu ujauzito wake na alifahamu kupitia tangazo la mtandao wa Instagram.

Beyonce amateuliwa kwa tuzo tisa za Grammy mwezi huu.

Tangazo lake la ujauzito kwa sasa ndilo maarufu zaidi katika mtandao wa Instagram likipendwa na watu milioni 9.

Beyonce ametoa picha zaidi akiwa ndani ya maji na nyingine akiwa ameketi juu ya gari kuu kuu.

Haki miliki ya picha Beyonce.com
Image caption Beyonce