Wasichana wenye sura mbaya watakiwa kulipa mahari zaidi India

Ulipaji mahari ni tamaduni ya miaka mingi kusini wa bara Asia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ulipaji mahari ni tamaduni ya miaka mingi kusini wa bara Asia

Kitabu kimoja cha shule katika jimbo la Maharashtra nchini India, kimezua ghadhabu baada ya kusema kuwa watu wenye sura mbaya wanastahili kulipa mahari zaidi.

Kitabu hicho kinasema kuwa ikiwa msichana ana sura mbaya au ni mlemavu, inakuwa vigumu kwa wasichana kama hao kuolewa na hivyo bwana harusi na familia yake huomba mahari zaidi.

Waziri mmoja alivyambia vyombo vya habari kuwa aya hiyo itaondolewa.

Picha za ujumbe huo zilisambazwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Ulipaji mahari na tamaduni ya karne nyingi kusini mwa bara Asia, ambapo wazazi wa bibi harusi hutoa pesa, nguo na vito vya thamania kwa familia ya bwana harusi.

Mizozo inaweza kuibuka kuhusu no pesa ngapi zinaweza kulipwa. Wakati mwingine wakati bwana harusi na familia yake hawalipwi, Bi harusi anaweza kudhulumiwa vibaya.