Miji inayowahifadhi wahamiaji kutozwa kodi kubwa Marekani

Sheria ya miji inayowahifadhi wahamiaji wengi kutozwa kodi kuwasilishwa kati bunge la seneti Marekani
Image caption Sheria ya miji inayowahifadhi wahamiaji wengi kutozwa kodi kuwasilishwa kati bunge la seneti Marekani

Kamati maalumu katika Bunge la Senet la Texas imeidhinisha mswada ambao utatoza faini kubwa miji inayowapa hifadhi wahamiaji na kukataa kuwakabidhi kwa maafisa wa usalama ili wasafirishwe.

Mswada huo unatazamiwa kuwasilishwa katika Bunge la Senet la Kitaifa, linalothibitiwa na wanachama wengi zaidi wa chama cha Republican mapema juma lijalo.

Mamia ya waandamanaji walipinga pendekezo hilo wakisema kuwa hatua hiyo itaimarisha ubaguzi wa rangi ambapo watu wengi watatiwa mbaroni kwa sababu ya asili zao.