Adama Barrow aongeza saa za kufanya kazi Gambia

Rais mpya wa gambia Adama Barrow
Image caption Rais mpya wa gambia Adama Barrow

Rais wa Gambia Adama Barrow amefutilia mbali sheria ya kufanya kazi siku nne kwa wiki ilioanzishwa na mtangulizi wake Yahya Jammeh.

Katika taarifa Adama Barrow amesema kuwa wafanyikazi wa serikali watalazimika kufanya kazi nusu siku ya Ijumaa pia .

Miaka minne iliopita Jameh alisema kuwa raia Waislamu nchini humo wanafaa kutumia siku ya Ijumaa kusali, kutembeleana na kulima.

Saa rasmi za kazi sasa itakuwa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni kutoka Jumatatu hadi Alhamisi ,na Ijumaa watu wataanza kufanya kazi saa mbili hadi saa sita na nusu siku ya Ijumaa hivyobasi saa hizo za kufanya kazi kuwa 36 na nusu kwa wiki.

Mwanadishi wa BBC Umaru Fofana anasema kuwa hatua ya kufanya kazi kwa siku nne kwa wiki ilikuwa na wakosoaji wake lakini chini ya serikali iliopita, ukosaji wa hadharini ungesababisha adhabu kali.