Ndege zatakiwa kubeba abiria wa nchi 7 za Waislamu kueleka Marekani

Kampuni ya ndege ya Qatar Airline
Image caption Kampuni ya ndege ya Qatar Airline

Idara ya forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.

Shirika la ndege la Ghuba, Qatar Airways, lilisema litaanza kupakia abiria haraka.

Raia wa mataifa 7 ya Waislamu sasa kuingia Marekani

Hatua hiyo inafuata saa tu baada ya jaji wa mahakama ya taifa ya Marekani, kuzuia amri hiyo ya Rais Trump kwa muda.

Mahakama iliamua kuwa hatua ya rais ilivunja katiba, ambayo inakataza dini moja kupendelewa kushinda nyengine.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanafunzi kutoka Iran aliyefurahishwa na hatu hiyo ya mahakama

Serikali inasema itakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Katika hotuba yake ya kila juma, rais alisema amri yake ilikusudiwa kuwalinda Wamarekani