Kanisa lamkosoa Duterte kwa mauaji

Rodrigo Duterte Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rodrigo Duterte

Kanisa katoliki nchini Ufilipino, limetaja kampeini ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya, inayoongozwa na Rais wa nchi hiyo, Rodrigo Duterte, kama ugaidi dhidi ya watu maskini.

Kanisa hilo linasema kuwa, inafahamika bayana kuwa, kuna upendeleo mkubwa miongoni mwa wanaouwawa.

Kufikia sasa maelfu ya watu wameuwawa katika jihudi hizo za Rais za kutaka kuangamiza magenge ya walanguzi na watumiaji wa mihadarati.

Ujumbe wa kanisa hilo umesomwa kote nchini Ufilipino leo Jumapili.

Tangazo hilo linakuja wiki moja tu baada ya Rais Rodrigo Duterte kuahirisha kampeini hiyo kutokana na ufisadi wa idara ya polisi.