Mlanguzi maarufu wa mihadarati akamatwa Mexico

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanajeshi hupambana na walanguzi wa mihadarati Mexico

Majeshi ya Mexico, yamemtia mbaroni kinara mmoja mkuu wa genge la Beltrán Leyva, la ulanguzi wa dawa za kulevya katika jimbo la Nuevo Leon, kaskazini mwa nchi hiyo.

Eleazar Palomo Castillo, maarufu kwa jina El Cochi au The Pig, anatajwa kuwa kama kiongozi mkuu wa mihadarati katika mji wa San Pedro Garza García, na naibu kamanda wa genge hilo katika jimbo hilo, linalo pakana na Marekani.

Taarifa kutoka kwa jeshi la Mexico zilisema kuwa alikamatwa baada ya gari lake kukataa kusimama kwenye kizuizi cha ukaguzi karibu na uwanja wa ndege wa Monterrey.