Theluji yaua zaidi ya watu 40 Afghanistan na Pakistan

Wakuu wa Afghanistan wanasema watu zaidi ya 40 wamekufa katika majimbo 19 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakuu wa Afghanistan wanasema watu zaidi ya 40 wamekufa katika majimbo 19

Theluji nyingi iliyoanguka sehemu za Afghanistan na Pakistan na miporomoko ya barafu, imeuwa watu kadha.

Wakuu wa Afghanistan wanasema watu zaidi ya 40 wamekufa katika majimbo 19, majimbo ya Parwan na Badakhshan ndiyo yameathirika zaidi.

Barabara kuu katika sehemu nyingi za Afghanistan hazipitiki, na uwanja wa ndege mkuu umefungwa.

Theluji nyingi iliyoanguka, imepelekea wakuu kutangaza leo kuwa siku ya likizo.

Na katika nchi jirani ya Pakistan, watu kama 13 wamekufa pale barafu ilipoporomoka na kuzika nyumba kadha.