Utafiti: IS inawasajili watoto wakimbizi

Wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq
Image caption Wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq

Watafiti nchini Uingereza wamebaini kuwa makundi yenye itikadi kali kama Islamic State yanawaingiza kwenye makundi hayo watoto wanaokimbia mizozo wakiwa peke yao.

Uchunguzi huo uliofanywa na wakfu unaochunguza fikra za itikadi kali unasema kuwa makundi hayo yanajaribu kuvutia ufuasi wa watoto katika kambi za wakimbizi kwa kuwalipa watu wanaowatorosha na kuwasafirisha hadi Ulaya

Ripoti yao inasema kuwa kundi kama Islamic State lina azma ya kuingiza fikra za itikadi kali katika vijana hao katika kila hatua ya safari yao .

Watafiti hao walibaini kuwa wengi miongoni mwa vijana wadogo wanaoomba uhamiaji wanawasili Marekani wakiwa peke yao na wanakuwa katika hatari ya kubakwa ama kutumiwa vibaya katika shughuli za kiuchumi.