Al-Shabab wawakata vichwa wapelelezi wa Marekani na Kenya

Wanaume hao walikatwa vichwa hadharani kwenye mji ulio walaya ya Jamame eneo la Jubba
Image caption Wanaume hao walikatwa vichwa hadharani kwenye mji ulio wilaya ya Jamame eneo la Jubba

Kundi la wanamgambo la al-Shabab la nchini Somalia, limethibitisha kuwa limewaua wanaume wanne waliolaumiwa kwa kuipelelezea Marekani, Kenya na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na nchi za magharibi.

Wanaume hao walikatwa vichwa hadharani kwenye mji ulio wilaya ya Jamame eneo la Jubba karibu kilomita 70, kaskazini mwa mji wa Kismayo baada ya kupatwa na hatia na mahakama ya Sharia.

Wanaume hao walikiri kuwa walikuwa wapelelezi, kwa mujibu wa shirika la Reuters, lililomnukuu gavana wa al-Shabab Abu Abdalla, eneo la Jubba.