Kompyuta ya LG yashindwa kufanyakazi na Wi-Fi

Image caption Tarakilishi aina ya LG Ultrafine 5K monitor

LG imekiri kwamba Ultrafine 5K monitor, haiwezi kufanya kazi ikiwa karibu na wi-fi.

Kampuni kubwa ya uundaji wa vifaa vya kielektroniki LG, imekiri kuwa tarakilishi yake mpya ya kuonyesha orodha ya bei ya mauzo, "ina matatizo ya kufanya kazi" hasa inapowekwa karibu na kifaa cha wi-fi.

Screen hiyo mpya ya LG Ultrafine 5K monitor, inayogharimu kiasi cha Dola 900, imepigiwa debe pakubwa kama kifaa cha nje cha kuonyeshea orodha ya bidhaa kwa Mac.

Lakini wateja wamegundua kuwa kuna matatizo katika maonyesho yake au hata kuzima kabisa inapokuwa karibu na kifaa cha wi-fi, huku nyingine zikionyesha taarifa potovu katika tovuti ya Apple.

LG imeiambia BBC kuwa wateja wanafaa kubadilisha sehemu ya kuonyeshea bidhaa zao.

"Tarakilishi hiyo inawasili leo na picha zinatatanika au kuzima na kuwaka inapotumia Laptopu mpya ya mkononi ya Macbook Pro," mchunguzi mmoja aliandika.

Mwingine alioneza kuwa: "kifaa hicho hakijalidwa ipasavyo kutokana na mionzi ya wi-fi, kwa hivyo inafaa kutoweka kifaa cha wi-fi kama mita mbili karibu nayo au itazima.

"Kwa hivyo haiko tayari kuuziwa umma."

Kwa njia ya taarifa, LG imeomba msamaha kwa "kuwatatiza wateja wake" kutokana na kile walichopitia.

"Kubadilisha sehemu au kuweka mbali kidogo kifaa cha Wi-fi, kunafaa kutanzua tatizo hilo". Imesema.

Kompyuta hiyo mpya ya Ultrafine 5K monitor, imeundwa mwezi huu wa Februari 2017.

Kampuni ya LG sasa inawaomba wateja wake, ikiwa kunaye ambaye atapata matatizo ya namna yoyote, awasiliano nayo.