Netanyahu na Theresa May wazungumzia tisho la Iran

Image caption Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ajadiliana na mgeni wake Benjamin Netanyahu osifini kwake

Waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May, amemwalika Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kwa mazungumzo katika ofisi yake iliyoko Downing Street, Jijini London.

Bi May ametaja wasiwasi wake dhidi ya ujenzi wa majengo mapya kwa walowezi wa kiyahudi magharibi mwa mto Jordan, ilihali Bw. Netanyahu alionya kuwa Iran inatoa tishio kwa mataifa ya bara Ulaya, baada ya kufanyia majaribio ya zana zake za kitonoradi. Huku akitoa mwito kwa hatua kali zichukuliwe.

Waziri mkuu wa Uingereza alishindwa kumsalimu kwa mkono mwenzake wa Israeli alipowasili baada ya kutokea hali ya sintoifahamu.

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Netanyahu akiwa Downing Street, Jijini London

Kwanza mkutano huo ulifanyika ana kwa ana kati ya viongozi hao wawili.

Mkutano huo unafanyika baada ya Uingereza kuunga mkono uamuzi wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa mwezi Disemba mwaka uliopita, kupinga hatua ya Israeli ya kujenga makao kwa walowezi wa kiyahudi, katika ardhi ya Wapalestina huku ikitaja hatua hiyo kama "ukiukaji wa wazi wa" wa sheria ya kimataifa na "kizuizi kikuu" kwa upatikanaji wa amani ya kudumu.