Kati ya Adam na Mohamed, ni nani atapata kazi?

Wasifu zilizotumwa zilikuwa na viwango sawa vya kuhitumi
Image caption Wasifu zilizotumwa zilikuwa na viwango sawa vya kuhitimu

Mtafuta kazi aliye na jina linalofanana na la kiingereza alipata fursa za kuhojiwa mara tatu zaidi kumliko mtafuta ajira ambaye alikuwa na jina la kiislamu kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na BBC.

Wasifu wa watafuta ajira wawili "Adam" na "Mohamed" ambao walikuwa na ujuzi sawa kitaaluma zilitumwa kwa ajira 100.

Adam aliitwa kwa mahojiano mara 12 huku Mohammed akipata nafasi nne tu.

Hii inamaanisha kuwa waislamu wanaoishi nchini Uingereza hawana fursa nyingi za kazi kama watu kutoka dini zingine.

'Nilitumia jina John Smith'

Image caption Yogesh Khrishna alishuku kuwa alidharauliwa kutokana na jina lake na akaamua kufanya majaribio yeye mwenyewe.

Yogesh Khrishna Davé, mweye umri wa miaka 56 ni mkurugenzi kwenye kampuni ya madawa. Anasema imemchukua miongo kadha kupata cheo alicho nacho.

Wakati wa miaka ya nyuma alishuku kuwa alidharauliwa kutokana na jina lake na akaamua kufanya majaribio yeye mwenyewe.

"Nilianza kazi miaka ya themanini na mara kwa mara nilipotuma wasifu wangu nilikataliwa."

Ndipo mtu mmoja akamshauri atumie jina la kiingerea kwenye wasifu wake la John Smith, na wasifu mwingine akatumia jina lake halisi Yogesh. John Smith aliitwa kwa mahojiano na yeye Yogesh akakataliwa.

Ripoti ya mwaka 2015 ilionyesha kuwa waislamu wanaoishi nchini Uingereza hawana uwakilishi katika nafasi za juu ikilinganishwa na dini zingine.