Kiir: ataka wanajeshi wanaobaka raia wauawe

Rais wa Sudan Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Sudan Kusini

Rais wa Sudan kusini Salva Kiir amesema wanajeshi ambao wanao baka raia wanapaswa kuuawa.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea mji wa Yei uliopo kusini magharibi mwa nchi hiyo, ikiwa kama sehemu ya juhudi za upatanishi katika maeneo yenye uhasama.

Kauli ya Rais Kiir ameitoa kufuatia tuhuma zinazotolewa na makundi ya haki za binadamu kwamba wanajeshi wamekuwa wakiwabaka wanawake.

Sudan kusini ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013, baada ya Rais Kiir kutoka kabila la Dinka alipomfukuza kazi Makamu wake Riek Machar kutoka jamii ya Nuer.

Ripoti kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia nchini humo imeongeza hali ya mvutano na wasiwasi kati ya serikali ya Sudan kusini na wafadhili kutoka nchi za magharibi.

Mada zinazohusiana