Bunge la Israel lahalalisha makaazi ndani ya ardhi ya Palestina

Makaazi ya Israel yaliojengwa katika ardhi inayomilikiwa na Palestina katika eneo la West Bank
Image caption Makaazi ya Israel yaliojengwa katika ardhi inayomilikiwa na Palestina katika eneo la West Bank

Kumekuwa na shutma nyengine za kimataifa zinazokosoa sheria mpya iliopitishwa na bunge la Israel ambayo inahalalisha maelfu ya makaazi ya Israel yaliojengwa katika ardhi ya Palestina huko West Bank.

Maafisa wa Palestina wanasema kuwa hatua hiyo inahalalisha wizi, huku afisa wa Umoja wa Mataifa akisema itaathiri matumaini ya kupata amani katika eneo hilo.

Marekani imesema kuwa haitatoa tamko lake hadi pale mswada huo utakapoangaziwa na mahakama za Israel, ambapo huenda ukapingwa.

Image caption Bunge la Israel limehalalisha makaazi ya ya Israel katika ardhi inayomilikiwa na Palestina

Mkuu wa Sheria amesema kuwa ni kinyume na katiba na kwamba hatautetea katika mahakama ya juu.

Sheria hiyo itasimamia nyumba 4000 huku wamiliki wake wa Palestina wakifidiwa.

Ni hatua za hivi karibuni zinazounga mkono makaazi zaidi ya Israel katika ardhi ya Palestina tangu rais Trump achukue mamlaka.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii