Bado ukeketaji tatizo Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Bado ukeketaji wa wasichana ni tatizo Kenya

Wakati bado dunia ikiendelea kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga mila ya ukeketaji, harakati na kampeni za kupinga mila hiyo potovu miongoni mwa jamii ya Wameru walio eneo la kati la Kenya imeanza kuzaa matunda.

Wengi wa Wanawake wakeketaji au Ngariba miongoni mwa jamii hiyo ya wameru sasa wameamua kuacha kabisa utamaduni huo na kuamua kutafuta kipato kwa njia mbadala.

Lakini, Mwandishi wetu Paula Odek alipotembelea eneo hilo la Meru aligundua kwamba sio kila mkeketaji yuko tayari kuachana na mila hiyo potovu.

Mada zinazohusiana