Amri ya kutotembea yatangazwa Mogadishu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mzozo wa tangu mwaka 1991 umeharibu majengo mengi mjini Mogadishu

Maeneo kadha ya mji mkuu wa Somalia Magadishu yamewekwa chini ya amri ya kutotembea, siku moja kabla ya wabunge wa kumchagua rais mpya.

Hatua hizo za kiusalama zinalenga maeneo yanayozunguka uwanja wa ndege eneo ambalo kura itafanyika, licha ya wasiwasi wa kuwa huenda kukatokea shambulizi kutoka kwa wanamgambo wa kiislamu wa al Shabab.

Marufuku ya safari za ndege kupitia maeneo fulani nayo imetangazwa. Somalia haijakuwa na serikala kamili tangu utawala wa Siad Barre uanguke mwaka 1991.