Aliyekuwa rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kufunguliwa mashtaka

Sarkozy alikuwa rais wa Ufaransa kati ya mwaka 2007-2012 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sarkozy alikuwa rais wa Ufaransa kati ya mwaka 2007-2012

Jaji mmoja nchini Ufaransa amemhamrisha rais wa zamani Nicolas Sarkozy, kufika mahakamani kujibu mashtaka yanayohusu matumizi ya pesa haramu katika kampeni ya uchaguzi alioshindwa mwaka 2012.

Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa Bwana Sarkozy alijaribu kukwepa kiasi cha pesa za kutumia katika kampeni kwa kutumia kampuni ya uhusiano bora, Bygmalion, kutoa risiti kwa chama chake badala ya kutoa risiti hiyo kwa kamati kuu ya kampeni yake, kwa kazi iliyofanywa katika kampeni yake.

Alishindwa kwenye uchaguzi huo na Francois Hollande na kushindwa tena kupata nafasi ya kuwania uchaguzi wa urais unaokuja.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sarkozy (kulia) alipoteza uchaguzi wa mwaka 2012 kwa Francois Hollande (kushoto)

Kesi hiyo inatarajiwa kuangazia ikiwa Bwana Sarkozy mwenye alikuwa akifahamu kuhusu fedha hizo.

Watu wengine 13 pia nao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Haya yanajiri wakati Francois Fillon amabye alimshinda Sarkozy na kuwa mgombea wa chama cha kati - kulia kwenye uchaguzi wa urais, kulaumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kumuajiri mkewe na wanawe wawili.