Maelfu wamenyongwa gerezani nchini Syria

Amnesty International inasema kuwa gereza la Saydnaya linaweza kuhifadhi kati ya watu 10,000 na 20,000 Haki miliki ya picha Amnesty International/Forensic Architecture
Image caption Amnesty International inasema kuwa gereza la Saydnaya linaweza kuhifadhi kati ya watu 10,000 na 20,000

Hadi watu 13,000 wengi wao wakiwa ni raia ambao ni wafuasi wa Upinzani wamenyongwa kwenye gereza la kisiri nchini Syria kwa mujibu wa shirika la Amnesty International

Ripoti mpya kutoka kwa shirika hilo la haki za bidamu inadai kuwa watu wengi walinyongwa kila wiki kwenyr gereza la Saydnaya kati ya mwezi Septemba mwaka 2011 na Disemba mwaka 2015.

Amnesty inasema kuwa mauaji hayo yaliamrishwa na watu wa ngazi za juu kutoka kwa serikali ya Syria.

Haki miliki ya picha Amnesty International
Image caption Mfungwa za zamani Omar al-Shogre kabla ya kukamatwa na baada ya kuachiliwa

Amnesty iliwafanyia mahojiano watu 84 wakiwemo walinzi wa maafisa wa gereza, wafungwa wa zamani na maafisa wa gereza la Saydnaya kwa ripoti yake.

Linadai kuw kila wiki au mara mbili kwa wiki, kundi la kati ya watu 20 na 50 walinyongwa kisiri ndani ya gereza hilo lililo kaskazini mwa mji wa Damascus.

Kabla ya kunyongwa wafungwa wangeletwa mbele ya mahakama ya kijeshi kuhukumiwa, shughuli iliyochukua kati ya dakika moja na tatu.

Image caption Syria

Kulingana na ripoti, wafungwa wangejulishwa wakati wa aiku ya kunyongwa kuwa wangehamishiwa gereza la kiraia lakini walipekwe korokorotni iliyo chini ambapo walipigwa kati ya muda wa saa mbili na tatu.

Kishaa usiku wa manane walifungwa macho na kuhamishiwa chumba kingine ambapo waliambiwa kuwa wamehukumiwa kifo muda mfupi kabla ya kuwekwa kamba shingoni.

Kisha maiti zao zilijazwa kwa malori na kusafirishwa kuenda hospitali ya kijeshi ya Tishreen, ambapo zilizikwa makaburi ya pamoja kwenye ardhi ya kijeshi.